KITENGO CHA UJENZI

Utangulizi:-
Kitengo cha Ujenzi ni mojawapo ya Vitengo vitatu vilivyopo chini ya Divisheni ya Huduma za Urekebishaji. Kulingana na Sheria namba nne (04) ya mwaka 1967 ambayo ilianzisha Jeshi la Magereza, inaelekeza kuwa lengo Kuu la Jeshi la Magereza ni kumhifadhi, kumrekebisha na kumjenga mfungwa kitabia ili pindi amalizapo kifungo chake aweze kuwa raia mwema. Hivyo kulingana na azma hiyo, Kitengo cha Ujenzi ni mahususi kwa urekebishaji wa tabia za wafungwa Magerezani.


Shughuli za Kitengo:-
● Kupunguza gharama kwa Serikali za ujenzi ambapo Jeshi linatumia wataalam wake wa ndani.
● Kutoa fursa kwa wafungwa kujifunza stadi mbalimbali za ufundi kwa vitendo ikiwa ni sehemu ya mpango wa urekebishaji.
● Ujenzi, Uimarishaji na upanuzi wa Majengo ya Magereza.
● Ujenzi wa Magereza mapya.
● Ujenzi na ukarabati wa nyumba za askari.
● Ukarabati na ujenzi wa mifumo ya maji safi na taka.
● Upimaji wa maeneo ya Magereza, kusimamia na kutoa miongozo ya ardhi ambayo ipo chini ya Jeshi la Magereza.
• Kuratibu mafunzo ya ngazi mbalimbali kwa wafungwa katika Chuo cha mafunzo ya ufundi kilichopo Ruanda Mbeya na Gereza la Wami Vijana lililopo Wami Morogoro.
• Kujenga na kukarabati majengo mbali mbali ya serikali, taasisi mbali mbali na watu binafsi kwa kandarasi kupitia Shirika la Magereza. Ili kukidhi matakwa ya kisheria.


Shirika la Magereza (Prisons Corporation Sole) linatambuliwa na limesajiliwa na Bodi ya usajili wa Makandarasi Nchini (Contractors Registration Board – CRB) tangu mwaka 2001 na sasa lipo katika Madaraja yafuatayo.

1. Ujenzi wa majengo mbalimbali daraja la kwanza (Class one).
2. Kazi za umeme daraja la tano (Class five)
3. Ujenzi wa barabara daraja la nne (Class four)

Kazi za Ukandarasi:-
Walengwa wa huduma hii ni Serikali, Taasisi za Serikali na za binafsi na Watu binafsi katika maeneo yafuatayo:-
1. Ujenzi wa majengo.
2. Ukarabati wa majengo.
3. Ujenzi na ukarabati wa mifumo ya maji safi na maji taka.
4. Kazi za umeme.
5. Kazi za “Landscaping”.
6. Ujenzi na ukarabati wa huduma za majengo kama, mifumo ya viyoyozi na mifumo ya tahadhari za moto.


Kwa kipindi cha miaka kumi (10) iliyopita kazi kubwa za ujenzi zifuatazo zilifanyika :-
● Ujenzi wa jengo la ghorofa nne la Ofisi ya Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – D’Salaam.
● Ukarabati mkubwa na upanuzi kwa kuongeza ghorofa za jengo la Wizara ya Sayansi, Teknolojia na elimu ya juu lililopo Mtaa wa Jamhuri - D’Salaam.
● Ukarabati wa jengo la Ofisi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lililopo Mtaa wa Luthuli – D’Salaam.
● Ujenzi wa jengo la ghorofa nne lenye vyumba vya madarasa na Ofisi la Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama – D’Salaam.
● Ujenzi wa Maabara ya Chakula ya Ofisi za TIRDO Msasani.
● Ukarabati wa jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza lililopo Mtaa wa Sokoine/Shaaban Robert – D’Salaam.
● Ujenzi wa Nyumba Hamsini za kuishi Watumishi wa Serikali daraja “A” zilizopo eneo la Kisasa – Dodoma.
● Ukarabati wa majengo ya Chuo cha Polisi yaliyopo Kidatu.
● Ujenzi wa msingi wa jengo la ghorofa litakalokuwa la Maktaba ya Chuo cha Usafirishaji (NIT) – Mabibo D’Salaam.
● Ujenzi wa maghorofa (Cluster 5) ya kuishi askari Polisi Kilwa Road, kila cluster moja likiwa na majengo matatu yaliyoshikana pamoja ambapo kila jengo lina ghorofa tatu.
• Ukarabati Mkubwa wa majengo ya Bunge huko Dodoma.

BAADHI YA MAJENGO YALIYOJENGWA AMA KUKARABATIWA NA KIKOSI CHA UJENZI

MOJAWAPO YA JENGO LA KUISHI ASKARI POLISI LILILOPO KURASINI D’SLAAM

JENGO LA OFISI YA IDARA YA WAKIMBIZI LILILOPO WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JENGO LILILOKUWA LA KUISHI WAFANYAKZI WA SHIRIKA LA POSTA NA SIMU AMBALO HIVI SASA NI OFISI YA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA BAADA YA KUKARABATIWA.

MOJA YA NYUMBA ZA KUISHI ASKARI MAGEREZA ZILIZOKO CHUO UKONGA, DAR-ES-SALAAM ZILIZOJENGWA KWA KUTUMIA MATOFALI YA HYDRAFARM.

.