MAISHA YA GEREZANI
Unapowasili gerezani

Mtu anapowasili gerezani anahojiwa na kuchunguzwa ili; Kuelewa sheria na taratibu za gerezani
Kuelewa haki zake, pamoja na Kupata huduma za afya zinazostahili.

Halafu mfungwa anapewa namba ya Kifungo na mali zake zinaingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu na kutunzwa kwa usalama mpaka atakapomaliza kutumikia kifungo chake.

Kwa maelezo zaidi bofya hapa

Huduma za Afya Magerezani

Wafungwa wanapewa huduma sawa za afya na matibabu kama anavyopata mtu mwingine yeyoto nje ya gereza. Matibabu ni bure ingawa ni lazima yaidhinishwe na Daktari wa Gereza

Mawasiliano
Wafungwa wanaruhusiwa kupokea wageni wa familia, marafiki na wawakilishi wa kisheria wanapokuwa gerezani.

Simu
Wafungwa hawaruhusiwi kuzungumza na kupokea simu za mkononi.

Barua
Wafungwa wanaruhusiwa kupokea na kupeleka barua. Barua zote ni lazima zikaguliwe ili kuhakikisha kuwa hazina vitu vilivyokatazwa/kupigwa marufuku au taarifa itakayohatarisha usalama na utulivu wa gereza.


Barua pepe, intaneti na mitandao ya kijamii.
Wafungwa hawaruhusiwi kutumia barua pepe, mitandao ya kijamii wala intaneti.
.