Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu, jijini Dar es Salaam wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Jeshi hilo leo. Masauni mara baada ya kumaliza ziara yake aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji nchini, kuanzia sasa sare zote za askari na maafisa wa Idara hizo zitashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Kwa habari picha zaidi tembelea www.magereza.blogspot.com