Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu, Oktoba 03, 2024 ambetembelea Ofisi za Wizara ya Fedha zilizopo Jijini Dodoma, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mipango ya maendeleo ya Jeshi la Magereza.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu (kushoto kwake), na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha akiwemo Kaimu Katibu Mkuu, Bi. Jenifa Christian Omolo (wanne kushoto) Viongozi waandamizi wa Jeshi la Magereza, baada ya kuhitimisha mazungumzo yao katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Jijini Dodoma.
CGP Jeremiah Yoram Katungu alifika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuliongoza Jeshi la Magereza, hivi karibuni.