"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua  SACP Mzee Ramadhan Nyamka, kaimu Kamishna wa Huduma za Urekebu, kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza.

SACP Ramadhan anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Uteuzi wa SACP Mzee Ramadhan Nyamka umeanza tarehe 24, Agosti, 2022" Ilieleza Taarifa kutoka kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Yafuatayo ni matukio mbalimbali kwa njia ya Picha yakimuonesha CGP.Nyamka baada ya kuteuliwa na kuapishwa kushika nafasi hiyo.

KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhan Nyamka, akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma, Agosti 29,2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Mzee Ramadhan Nyamka, kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), katika hafla fupi iliyofanyika Agosti 29,2022 Ikulu jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhan Nyamka, mara baada ya kumuapisha, Agosti 29,2022 Ikulu jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mzee Ramadhan Nyamka mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, Agosti 29,2022 Ikulu jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mzee Ramadhan Nyamka, akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa chuo cha Mafunzo Zanzibar, Hamis Bakari Hamis (kushoto), sambamba na Maafisa wengine kutoka Zanzibar walioalikwa kushuhudia tukio la kuapishwa Jenerali Nyamka, Agosti 29,2022 Ikulu jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Christopher Kadio, akimpongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP. Mzee Ramadhan Nyamka, mara baada ya kuapishwa Ikulu Chamwino, jijini Dodoma, Agosti 29,2022

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Maduhu Kazi, akimpongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP. Mzee Ramadhan Nyamka, mara baada ya kuapishwa Ikulu Chamwino, jijini Dodoma, Agosti 29,2022

KAMISHNA Jenerali mpya wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhan Nyamka, akipokea salamu kutoka kwa gwaride la heshima, lililoandaliwa kwaajili yake, mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato jijini Dodoma, Agosti 29,2022.

KAMISHNA Jenerali mpya wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhan Nyamka, akikagua gwaride la heshima, lililoandaliwa kwaajili yake, mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato jijini Dodoma, Agosti 29,2022.

KAIMU Kamishna wa utawala na rasilimali watu wa Jeshi la Magereza (DCP) Jeremiah Katungu (kushoto), akikabidhi baadhi ya nyaraka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Mzee Ramadhan Nyamka, mara baada ya kuwasili ofisini Makao Makuu ya Magereza, eneo la Msalato jijini Dodoma, Agosti 29,2022.

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Mzee Ramadhan Nyamka, akisoma kwa makini nyaraka aliyokabidhiwa mara baada ya kuwasili ofisini Makao Makuu ya Magereza, eneo la Msalato jijini Dodoma, Agosti 29,2022.

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Mzee Ramadhan Nyamka, akiwahutubia Maafisa, Askari na watumishi raia wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu ya Magereza , msalato jijini Dodoma. Jenerali Nyamka alitumia nafasi hiyo kutoa mwongozo wa uongozi wake mara baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo ya uongozi Ikulu Chamwino jijini Dodoma,Agosti 29,2022.