Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala amefanya ziara ya kikazi Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza zilizopo Msalato Jijini Dodoma, kwa lengo la Kujifunza maswala mbalimbali ikiwemo Miradi ya Ujenzi.

Aidha kamishna wa Jeshi la Uhamiaji Dkt Anna Makakala amempongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleimani Mzee kwa usimamizi mzuri wa miradi unaotekelezwa na Jeshi hilo.

" Mimi ninashangaa kila sehemu ninayokwenda ninaona mambo mengi mazuri na niwapongeze wewe na timu yako, mimi nakuja kidogo kidogo na ninaomba muongozo wako ili na sisi tuweze kufanikiwa maswala mbalimbali" Alisema CGI Dkt. Makakala

hata hivyo CGI Dkt. Makakala alisema kuwa sasa wanakiwanda cha ushonaji Nguo ambapo kwa siku wanashona pea Ishirini,pia amemuomba CGP wataalamu

Awali CGP Suleiman Mzee alimweleza CGI Dk.Makakala jinsi alivyoweza kufanikisha miradi mbalimbali katika Jeshi,alimweleza kuwa alisimamisha shughuli binafsi zinazofanywa na Askari katika maeneo ya Jeshi Kama kilimo na mifugo kutokana na matumizi mabaya ya rasilimali zilizopo.

"Mimi sikufahamu Kama Magereza Kuna wasomi wa kufa mtu wapo na hawatumiki,na Mimi sikutafuta toka nje wataalam wowote huku Kuna Kila aina ya wasomi wapo wa Kila aina"alisema CGP Mzee.