UHUSIANO NA NCHI ZA NJE |
Jeshi la Magereza Tanzania ni miongoni mwa wachangiaji wa Maofisa warekebishaji kwenye shughuli za utunzaji wa Amani Umoja wa Mataifa katika eneo la urekebishaji. Kuanzishwa kwa huduma hii ni katika kutimiza mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa urekebishaji unaohitaji nchi zinazoshiriki katika shughuli za utunzaji wa amani kutoa wataalamu wenye ujuzi wa kufufua Taasisi za Magereza zilizobomolewa katika nchi zilizopigana. Jeshi la Magereza lilianza shughuli za kutunza amani za umoja wa Mataifa mwaka 2009 kwa kupeleka Maofisa kwenye maeneo yaliyopigana kama vile Kongo, Liberia pamoja na Sudani ya Kusini na Sudan. Aidha ushirikiano na huduma nyingine za urekebishaji barani Afrika katika Programu za kubadilishana wataalamu kwenye Mafunzo kama vile Malaysia, Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia. Jeshi la Magereza Tanzania limefanya mikataba ya Uhamishaji wa wafungwa na nchi za Mauritius, Zambia, Namibia pamoja na Thailand. |
. |