UTANGULIZI Shirika la Magereza lilianzishwa mwaka 1983 kwa Sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 1974 (the Corporation Sole Act No. 23/1974) chini ya kifungu cha 3(1) na kanuni zake za mwaka 1983.
DIRA Shirika linajizatiti kuendesha shughuli zake kibiashara kuzalisha mali kwa ubora katika mzingira ya ushindani ili kupata faida.
MWELEKEO Bado tunalo lengo la kuboresha zaidi miradi ya Shirika ili iwe na uwezo kiuzalishaji na kuimarisha manejimenti ya miradi katika mwelekeo wa kuwa na miradi yenye tija na ufanisi.
MALENGO (i) Chombo cha urekebishaji wafungwa kuwafundisha stadi za kazi na kuwaongezea ujuzi kwa wale ambao tayari wana ujuzi.
(ii) Kuendesha shughuli zake kiuchumi na kibiashara kwa kujitegemea (Revolving fund).
(iii) Kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama za uendeshaji wa Magereza.
Muundo wa Shirika Muundo wa Shirika la Magereza ni kama ifuatavyo:-
VITENGO VYA SHIRIKA 1. Ujenzi na Ukarabati 2. Kilimo, Mifungo na Mazingira. 3. Viwanda vidogovidogo.
Miradi ya Shirika Shirika lina jumla ya Miradi 23, kati ya hiyo miradi 15 ni ya kilimo na mifugo na 8 ni ya viwanda vidogo vidogo, pia zipo shughuli za mradi wa Kikosi cha Ujenzi zinazosimamiwa na Shirika.
(i) Miradi ya Kilimo na Mifugo
1 |
Mradi wa Maziwa KPF |
S.L. P 11 Morogoro |
2 |
Mradi wa Nyama Mbigiri |
S.L.P 65 Morogoro |
3 |
Mradi wa Mahindi Songwe |
S.L.P 525 Mbeya |
4 |
Mradi wa Kilimo na Mifugo Kitengule |
S.L.P 96 Kyaka Kagera |
5 |
Mradi wa Mitamba Mugumu |
S.L.P 22 Mugumu |
6 |
Mradi wa Kilimo Mollo |
S.L.P 52 Sumbawanga |
7 |
Mradi wa Kilimo Ludewa |
S.L.P 11 Ludewa |
8 |
Mradi wa Kilimo na Mifugo Isupilo |
S.L.P 1 Mafinga |
9 |
Mradi wa Kilimo Kiberege |
S.L.P 76 Mang'ula |
10 |
Mradi wa Kilimo Idete Morogoro |
S.L.P 125 Ifakara |
11 |
Mradi wa Kilimo Kitai |
S.L.P 391 Songea |
12 |
Mradi wa Kilimo Mkwaya |
S.L.P 12 Mbinga |
13 |
Mradi wa Kilimo Bagamoyo |
S.L.P 92 Bagamoyo |
14 |
Mradi wa Kilimo Mang’ola |
S.L.P 36 Karatu |
15 |
Mradi wa Kilimo Arusha |
S.L.P 369 Arusha |
(ii) Miradi ya viwanda vidogo vidogo
1 |
Kiwanda cha Ushonaji Ukonga |
S.L.P 9091 Dar es Salaam |
2 |
Mradi wa Viatu Karanga |
S.L.P 237 Moshi |
3 |
Mradi wa Uhunzi KPF |
S.L.P. 25 Morogoro |
4 |
Mradi wa Mbao Uyui |
S.L.P 9 Tabora |
5 |
Mradi wa Samani Arusha |
S.L.P 369 Arusha |
6 |
Kiwanda cha Seremala Ukonga |
S.L.P 9091 Dar es salaam |
7 |
Mradi wa Sabuni Ruanda |
S.L.P 1038 Mbeya |
8 |
Mradi wa Chumvi Lilungu |
S.L.P 240 Mtwara |
|