Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Katungu, Oktoba 11, 2024 ameshiriki katika Mahafali ya 21 ya Kidato cha Nne, Shule ya Sekondari Bwawani, inayomilikiwa na Jeshi la Magereza iliyopo Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani.

Akizungumza katika Mahafali hayo CGP. Katungu amewataka Wahitimu kwenda kutenda mema katika jamii na kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya ili wasije kujikuta katika mikono ya Sheria.

Aidha amewasihi wahitimu hao kufanya maandalizi mazuri wanapoelekea katika Mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne.

Mahafali hayo ya 21 ya Kidato cha Nne 2024 yamejumuisha wanafunzi 115, Wavulana wakiwa 71 na Wasichana 44.