Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka (kulia) akimkabidhi CGP. Jeremiah Yoram Katungu Hati ya Makabidhiano ya Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza, wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Magereza Msalato jijini Dodoma, Agosti 05, 2024. Hafla hiyo imefanyika siku chache baada ya CGP. Katungu kuteuliwa na kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza Julai 28, 2024 na kuapishwa Julai 31, 2024.
Hafla ya Makabidhiano ya Ofisi ilitanguliwa na Mapokezi rasmi ya CGP. Katungu, ikiwa ni mara ya kwanza kuwasili Makao Makuu ya Magereza tangu alipoteuliwa na kuapishwa kushika nafasi hiyo ya uongozi na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Nchini.
CGP. Katungu akipokea Salamu ya Heshima inayotolewa na Gwaride Maalum wakati wa hafla ya mapokezi mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Magereza.
Mara baada ya Mapokezi na Makabidhiano kukamilika, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Katungu, alizungumza na Maafisa, Askari na Watumishi wasio askari wa Jeshi la Magereza ambapo pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi kwakuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Kudumisha nidhamu na ushirikiano mahala pa kazi ili kuleta ufanisi wa kiutendaji.
Maafisa, Askari na Watumishi wasio askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza kwa makini CGP. Katungu.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu akiwa katika picha ya pamoja na CGP. Mstaafu Mzee Ramadhani Nyamka, na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, mara baada ya kukamilika kwa zoezi la Makabidhiano ya Ofisi ya Kamishna Jenerali, Agosti 05, 2024, jijini Dodoma.