KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP. Mzee Ramadhani Nyamka Oktoba 27, 2023 amefunga Mafunzo ya Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) kozi namba 12 iliyojumuisha Askari 114, Wanawake wakiwa Ishirini huku watano miongoni mwao ni Askari kutoka Chuo cha Mafunzo Zanzibar.

CGP. Nyamka amewataka Askari hao kufanya kazi kwa weledi na kutokiuka Taratibu, Kanuni na Miongozo ya Jeshi la Magereza huku akisisitizia suala la nidhamu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria za Nchi.

KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP. Mzee Ramadhani Nyamka, akikagua Gwaride Maalumu la Askari wanaohitimu Mafunzo ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo iliyofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam.