RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Machi 25, 2022 amezindua na kuweka mawe ya msingi katika Miradi mbalimbali ya Jeshi la Magereza Makao Makuu Msalato Jijini Dodoma, ambapo ameupongeza uongozi wa Jeshi kwa jitihada kubwa zinazoendelea kufanyika, katika kuanzisha na kuendeleza Miradi mbalimbali.