DCP. Jeremia Katungu, kwaniaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee, mwishoni mwa mwezi Februari amepokea ujumbe wa Wanafunzi 30 na Wakufunzi 43 wa Mataifa mbalimbali kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), ambao wametembelea Makao Makuu ya Magereza kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu Jeshi la Mgereza Tanzania Bara.

 

Mara baada ya kuwasili ujumbe huo wa Watu 73 kutoka NDC, uliendeshwa Mdahalo katika ukumbi wa Meja Gen Mzee, uliopo Magereza Makao Makuu, mdahalo uliohudhuriwa na Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, na kufuatiwa na kipindi cha maswali na majibu lengo likiwa ni kutanua uelewa wa Wanafunzi hao kuhusu namna Jeshi la Magereza linavyojiendesha.

 

Mara baada ya Kumalizika kwa Mdahalo huo, kulifuatiwa na zoezi la kupanda Miti na kutembelea Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Jeshi la Magereza Makao Makuu, ikiwemo Kiwanda cha kutengeneza Samani Msalato, Karakana na kuhitimishwa katika kituo cha kibiashara Isanga (ISANGA BUSSINESS CENTRE), ikifuatiwa na neno la shukrani kutoka Pnde zote mbili, na utoaji wa zawadi na kisha kuhitishwa rasmi kwa Ziara hiyo .

Msafara wa Wanafunzi na Wakufunzi kutoka NDC, uliongozwa na Brigedia Jenerali C.E. Msola.