Kaimu Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Magereza DCP. J. Katungu, Jana Januari 10, 2022, amefungua Mafunzo ya Maopareta wa Radio call wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.

Akizungumza wakati ufunguzi huo DCP. Katungu amewataka Maopareta hao kufuata misingi ya kazi hiyo ikiwemo utunzaji wa Siri za Ofisi.

"Mafunzo haya tunayafanya kwa nia nzuri, kumekuwa na baadhi ya Maopareta kufanyakazi kwa kukiuka maadili ya fani hii, hasa katika utunzaji wa Siri za Ofisi, Sasa kupitia Mafunzo haya sitarajii kuona makosa hayo yakijirudia, na nikisikia aliyefanya kosa Hilo ni mmoja Kati ya watu waliohudhuria Mafunzo, kwakweli tutamchukulia hatua Kali" amesema Katungu.

Katika Mafunzo hayo kumekuwepo na watoa mada mbalimbali akiwemo Opareta mstaafu, mkaguzi msaidizi wa Magereza H. Maisha, ambaye alitoa uzoefu wake katika fani hiyo, huku akiwataka Maopareta kufanya kazi kwa kufuata miiko ya taaluma hiyo.

Mafunzo hayo ya Siku Mbili yamefungwa Leo Januari 11, 2022 na Kaimu Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Magereza DCP. J. Katungu, ambapo ameahidi kuwa Jeshi litashughulikia maslahi ya maopareta, huku akisisitizia Usiri katika kazi hiyo nyeti ndani ya Jeshi.