Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Musa Kaswaka (kulia) akiwa na Meneja Uendeshaji wa Biashara wa Platnam Julius Mawinda(wa pili kulia) pamoja na maofisa michezo wa Jeshi,wakionesha baadhi ya jezi zilizokabidhiwa leo tarehe 11 Disemba 2018 na Taasisi ya Platnam Makao Makuu ya Jeshi la Magereza. Wa pili toka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Makusanyo wa Platnam Matana Maduhu.

Na Moses Sebastian Taasisi ya kifedha ya Platnam Limited inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa watumishi wa Umma na binafsi imegawa vifaa mbalimbali vya michezo kwa Jeshi la Magereza ili viwasaidie katika michezo ya Majeshi inayotarajia kuanza mwezi Februari 2019.

Akimkabidhi vifaa hivyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Musa Kaswaka,Meneja uendeshaji wa biashara Julius Mawinda alisema kuwa vifaa alivyoleta leo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za upungufu wa vifaa kwa Jeshi la Magereza kwenye mashindano hayo.

“Tutaongeza vifaa vingine baada ya wiki kadhaa ili timu iweze kutokana kabisa na changamoto ya vifaa vya michezo katika michezo hiyo” Alisisitiza Meneja Julius.

Akiongea kwa niaba ya Kamishna Jenerali,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Musa Kaswaka alimshukuru Meneja uendeshaji wa biashara Julius kwa kuendelea kulijali Jeshi kwa kulipatia vifaa hivyo ambavyo vitaisaidia timu kwenye michezo hiyo.

“Tunashukuru sana kwa kutupatia vifaa hivi na tunaomba msikwamie hapo kwani Jeshi linashiriki katika michezo mingi na linahitaji ‘sapoti’ kutoka kwenye taasisi kama yenu” Aliongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Kaswaka.

Vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na seti mbili za jezi ya kijani na nyeupe ambazo zitatumika kwenye michezo ya mpira wa wavu(volley ball) na mpira wa mikono(hand ball).

Baadhi ya vifaa vilivyoahidiwa kuletwa hapo baade ni pamoja na shinigads( vikinga ugoko),soksi na mipira.

Taassi ya Platnam imekuwa mdau wa siku nyingi na muhimu katika kusaidia shughuli mbalimbali za Magereza na hasa zile zinazohusu michezo.