Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akifuatilia kwa makini mazungumzo kati yake na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali, Martin Busungu(kulia) alipomtembelea Ofisini kwake leo Julai 20, 2018 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha rasmi tangu aapishwe rasmi kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, Julai 14, 2018. 

(Picha na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya  Jeshi la Magereza)

Na mwandishi wetu, Magereza

Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa wameahidi kushirikiana katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kupitia mashirika yake ya Magereza Corporation Sole na SUMA-JKT.

Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike alipomtembelea Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Matin Busungu ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa tangu ateulie kuwa mkuu wa Jeshi hilo Julai13, 2018.

Katika mazungumzo yao, wakuu hao wa taasisi hizo muhimu nchini wameonesha utayari wa ushirikiano katika miradi ya ujenzi pale taasisi moja inapokuwa na miradi mikubwa inayoweza kuhitaji utaalam au nguvu ya kuweza kushirikiana.

Aidha, Meja Jenerali Busungu amesema kuwa JKT lipo tayari kulikopesha matrekta Jeshi la Magereza wakati litakapokuwa limekamilisha mpango wake kilimo cha kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

“Namshukuru sana Meja Jenerali Busungu kwa kuonesha utayari wa kushirikiana na Jeshi la Magereza, kilichobaki ni kujipanga na kuanza utekelezaji mara moja”. Amesema Jenerali Kasike.

 

Kwa habari picha zaidi tembelea www.magereza.blogspot.com