Kamishna Mkuu Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Kamanda Simon A. Mwanguku akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu.

 

Kamishna Msaidizi wa Mwandamizi wa Magereza (SACP) Mstaafu  Mtiga Hussein Omari aagwa na kuziwa rasmi katika makaburi ya Kijitonyama Jijini Dar es salaam.
SACP Mtiga Omari alifariki tarehe 07. 08. 2017 katika Hosiptali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Marehemu SACP Mtiga alizaliwa tarehe 25.09.1956 katika kijiji cha Chumbi Kata ya Rusembe Tarafa ya Muhoro wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.

Alijiunga na Jeshi la Magereza mwaka 1979 akitokea Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alilojiunga nalo kwa mujibu wa sheria baada ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita (VI) katika shule ya sekondari ya wavulana Tabora (Tabora Boy’s)

Marehemu Mtiga alipata mafunzo ya ndani na nje ya kwa ngazi na nyakati tofauti ikiwa ni pamoja na Mafunzo ya Uongozi Dara la Pili na la Juu kutoka Chuo cha Maafisa  wa Magereza Ukonga (kwa sasa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Stashahada ya Uandishi wa Habari kutoka TSJ na Stashahada ya Uhusiano wa Kimataifa katika chuo cha Diplomasia Kurasini.

Mafunzo mengine ni Intelligence Security kutoka chuo cha Galilee nchini Israel na mafunzo mafupi kama vile Correctional Intelligence Management,Diplomatic Security Services nakadhalika.

SACP Mtiga ndani ya Jeshi la Magereza alifanya kazi katika vituo tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na Singida, Iringa,Uyui Tabora,Tarime na Musoma Mara na Makao Makuu kwa nyakati tofauti. Marehemu Mtiga nakumbukwa zaidi akiwa Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia na Operesheni, Habari na Msemaji wa Jeshi la Magereza.

Marehemu alistaafu kazi rasmi mwezi 07.2016 akiwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Kagera (RPO). Ameacha na watoto watano.Wakiume watatu na wakike 2.
Kamishna Jenerali wa Magereza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE.

Kwa habari picha zaidi tembelea www.magereza.blogspot.com