Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa Maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao. 

 

Kwa habari picha zaidi tembelea www.magereza.blogspot.com