HABARI MPYA Habari zaidi

 Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Magereza nchini limeokoa jumla ya Shilingi Bilioni 11, ikiwa ni gharama ya chakula cha wafungwa tangu lianze kujitegemea kwa chakula ikiwa  ni maelekezo ya Rais  Dkt. John Pombe Magufuli ya kulitaka jeshi hilo litumie nguvu kazi ya wafungwa ilionao kuzalisha chakula.

Akizungumza leo katika ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,iliyofanyika katika Makao Makuu Mapya ya Jeshi hilo ,Msalato jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee amesema walikuwa wanatumia Shilingi Bilioni Moja kila mwezi kulipa wazabuni wa chakula waliokuwa wanaliuzia chakula  jeshi hilo.

“Sasa hivi tunajitegemea asilimia kubwa kwa chakula, Serikali kabla ya mwezi wa tatu mwaka jana kila mwezi kulikua kuna deni la Bilioni Moja, lakini baada ya mwezi huo wa tatu sasa tunaokoa kiasi hicho cha fedha shilingi bilioni moja na mpaka sasa tuna miezi kumi na moja tunajilisha wenyewe kupitia shirika la magereza” alisema CGP Mzee

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo alilipongeza Jeshi la Magereza kwa kutekeleza vyema agizo la Rais Magufuli ikiwa sambamba na ujengaji wa kiwanda kikubwa cha samani ambapo mpaka kukamilika kwake kitagharimu shilingi Bilioni 1,101,743,123/=

“Niwapongeze kwa hatua mbalimbali za maendeleo ambazo zingine nimeshuhudia mwenyewe,lakini kubwa kuweza kujitegemea kwa chakula cha wafungwa hali iliyopelekea kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinabaki humu humu ndani na mnakitumia kwa shughuli zingine za maendeleo hongereni sana” alisema Naibu Waziri Chilo

HISTORIA YA JESHI LA MAGEREZA TANZANIA BARA

1.0.Utangulizi Jeshi la Magereza lilianzishwa rasmi mwezi Agosti 25,1931 baada ya mgawanyo wa majeshi ya Polisi na Magereza kutokea. Licha ya kuwa na majukumu ya kulinda usalama na mali za wageni, kabla ya mwaka 1931 Jeshi la Polisi lilifanya pia kazi za Magereza kama zilivyokuwa kwa tafsiri na madhumuni ya wakoloni. Jeshi la Magereza wakati lilipoanzishwa liliitwa Idara ya Jela ambapo shughuli zake zilibaki kuwa zile za kikoloni za utesaji wa wafungwa pamoja na kazi ngumu bila kujali kama ni ya manufaa kwao au kwa Taifa.

2.0 Dira na dhima ya Jeshi la Magereza

Jeshi la Magereza katika miaka ya 1990 lilianzisha dira na dhima yake kulingana na mabadiliko mbalimbali yaliyojitokeza.Dira ya Jeshi la Magereza ni kuwa Jeshi la kurekebisha wahalifu lenye utaalam wa hali ya juu linaloendeshwa katika kanuni na viwango vilivyowekwa Kitaifa na Kimataifa.

Dhima ya Jeshi la Magereza ni kutekeleza wajibu ipasavyo katika kuimarisha ulinzi wa jamii kupitia usimamizi wa kifungo na kuwasimamia wahalifu, huduma za mahabusu, programu na huduma zinashughulikia mahitaji ya urekebishaji wa wahalifu na ushauri wa Sera kuhusu uzuiaji wa uhalifu na ushughulikiaji wa wahalifu. Soma zaidi>>